Psalms 94

Mungu Mlipiza Kisasi Kwa Ajili Ya Wenye Haki


1 aEe Bwana, ulipizaye kisasi,
Ee Mungu ulipizaye kisasi, uangaze sasa.

2 bEe Mhukumu wa dunia, inuka,
uwalipize wenye kiburi kama wanavyostahili.

3 cHata lini, waovu, Ee Bwana,
hata lini waovu watashangilia?


4 dWanamimina maneno ya kiburi,
watenda mabaya wote wamejaa majivuno.

5 eEe Bwana, wanawaponda watu wako,
wanawaonea urithi wako.

6 fWanamchinja mjane na mgeni,
na kuwaua yatima.

7 gNao husema, “Bwana haoni,
Mungu wa Yakobo hafahamu.”


8 hSikizeni, enyi wajinga miongoni mwa watu;
enyi wapumbavu, lini mtakuwa na hekima?

9 iJe, aliyeweka sikio asisikie?
Aliyeumba jicho asione?

10 jJe, anayeadhibisha mataifa asiadhibu?
Je, awafundishaye wanadamu asiwe na maarifa?

11 k Bwana anajua mawazo ya mwanadamu;
anajua kwamba ni ubatili.


12 lEe Bwana, heri mtu anayeadhibishwa na wewe,
mtu unayemfundisha kwa sheria yako,

13 munampa utulivu siku za shida,
mpaka shimo litakapokuwa limechimbwa
kwa ajili ya mwovu.

14 nKwa kuwa Bwana hatawakataa watu wake,
hatauacha urithi wake.

15 oHukumu itasimamishwa tena kwenye haki,
wote walio na mioyo minyofu wataifuata.


16 pNi nani atakayeinuka dhidi ya mwovu kwa ajili yangu?
Ni nani atakayenikinga dhidi ya watenda maovu?

17 qKama Bwana asingelinisaidia upesi,
ningelikuwa ninaishi katika ukimya wa kifo.

18 rNiliposema, “Mguu wangu unateleza,”
Ee Bwana, upendo wako ulinishikilia.

19 sWakati wasiwasi ulipokuwa mwingi ndani yangu,
faraja yako ilinipa furaha nafsini mwangu.


20 tJe, kiti cha utawala wa udhalimu kitajiunga nawe,
ule utawala uletao taabu kutokana na sheria zake?

21 uHuungana kuwashambulia wenye haki,
kuwahukumu kufa wasio na hatia.

22 vLakini Bwana amekuwa ngome yangu,
na Mungu wangu amekuwa mwamba ninaoukimbilia.

23 wYeye atawalipa kwa ajili ya dhambi zao
na atawaangamiza kwa ajili ya maovu yao;
Bwana Mwenyezi Mungu wetu atawaangamiza.
Copyright information for SwhKC